Mbowe Afanyiwa Upasuaji wa Mguu Katika Hospitali ya Agakhan
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amefanyiwa upasuaji wa mguu wake alioumia baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kimeeleza kuwa tayari Mbowe amefanyiwa upasuaji huo na anaendelea vizuri na matibabu.
Mbowe ambaye amelazwa katika hospitali ya Agakhan akiendekea na matibabu ya mguu huo ambao unadaiwa kuvunjwa na watu waliomvamia wakati akiingia nyumbani kwake Dodoma.
Kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Hai alivamiwa Juni 9, 2020 na watu watatu wasiojulikana na kuushambulia mguu huo na kumsababishia majeraha majira ya saa sita usiku.
Mbowe alipekekwa hospitali na kupatiwa matibabu ya awali na kuhamishiwa katika hospitali ya Agakhani jijini Dar es Salaam.
No comments