Header Ads

Header ADS

Rapper Snoop Dogg Atoboa SIRI "Notorious B.I.G Aliumia Sana Nilipompa Taarifa ya Kifo cha 2PAC"

Licha ya kutoka pande tofauti za Marekani ambazo ziliingia kwenye matatizo na uhasama kimuziki miaka ya 90, rapper Snoop Dogg (West) na Notorious B.I.G (East) waliendeleza urafiki wao, na pia haikumfanya Biggie asitoe chozi baada ya kifo cha hasimu wake Tupac Shakur.

Kwenye mahojiano na Fatman Scoop, Snoop Dogg alikuwa akizungumza na B.I.G na hata baada ya Tupac Shakur kuuawa kwa kupigwa risasi, walikutana na kuzungumza. B.I.G alionesha kuguswa na kifo cha Pac na alionesha wazi machoni kwamba ameumia

"Nilimkuta nyumbani, alikaa kando ya kitanda na tulianza kuongea. Kisha alinitazama usoni na alionesha kusema kitu, alihuzunishwa kwamba Tupac amefariki, lakini nilimpotazama machoni niliona kabisa ameumizwa." alisema Snoop.

"Huyu sio jamaa ambaye angekuwa na furaha, huyu ni jamaa ambaye alimpoteza rafiki, walikuwa na tofauti na hakutakiwa kuhukumiwa kwa hisia zake. Alinielezea ni jinsi gani alimpenda Tupac." alisema Snoop.

No comments

Powered by Blogger.