Polisi Wengine Watatu Washtakiwa Kwa Kumuua George Floyd
Mwanasheria Mkuu wa Minnesota, Keith Ellison ametangaza kuwa maafisa watatu wa Polisi waliokuwepo wakati George Floyd anakandamizwa shingoni hadi kufariki wamefunguliwa mashtaka
Thomas Lane (37), J. Alexander Kueng (26) na Tou Thao (34) wameshtakiwa kusaidia mauaji ya daraja la pili. Mashtaka ya Afisa aliyemuwekea goti Floyd, Derek Chauvin yamebadilishwa na sasa anatuhumiwa kwa mauaji ya daraja la pili
George Floyd alifariki dunia baada ya Chauvin kumkandamiza na goti shingoni huku maafisa wengine wakishuhudia. Mara baada ya kifo chake, Polisi hao wote walifukuzwa kazi lakini Chauvin pekee alishtakiwa kwa mauaji
Baada ya wote wanne kushtakiwa, Mwanasheria wa familia ya Floyd, Benjamin Crump amesema hii ni hatua kubwa kuelekea kupata haki na wamefarijika kwamba uamuzi huo umetolewa kabla George hajazikwa
No comments