Header Ads

Header ADS

Kala "Bado Sijapata Dili Lolote la Uchaguzi ila Kwenye Jina la Lowassa toa Weka Magufuli.....



Msanii na mwanaharakati Kala Jeremiah amesema kuwa, kampeni za mwaka 2015 alimpigia Edward Lowassa, ila mwaka huu amesema pale kwenye jina la Lowassa atatoa na kuweka John Pombe Magufuli.

Akipiga stori kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio Kala Jeremiah amesema, "Mimi sio mwanasiasa ila ni mwanaharakati, kuna viongozi nawakubali na wengine pia siwakubali na sijapata dili lolote kwenye ishu za uchaguzi mwaka huu kwa hiyo sina presha" amesema Kala Jeremiah.

"Uchaguzi uliopita nilimpigia kampeni Lowassa, ila huu wa sasa hivi pale kwenye jina la Lowassa toa weka Magufuli, maana anayoyafanya ndiyo nilikuwa nataka kiongozi afanye" ameongeza.


No comments

Powered by Blogger.