PICHA :Tayari mwili wa Dereva wa Lori ambaye alitumbukia Mto Wami, Chalinze Umepatikana
Tayari mwili wa Dereva wa Lori ambaye alitumbukia Mto Wami, Chalinze baada ya Lori kufeli breki umeopolewa na Jeshi la Uokoaji na Zimamoto wakishirikiana na wavuvi, Timu ya Uokoaji imesema mwili umeharibika kwakuwa umekaa chini ya maji kwa zaidi ya siku tatu tangu Ijumaa June 05.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete @ridhiwani_kikwete ni miongoni mwa waliokuwepo Wami wakati mwili ukiopolewa, tayari gari la JWTZ Iimesaidia kuubeba mwili huo pamoja na Ndugu ili kuuwaisha kwenda kuuzika.
Zoezi la kulitoa Lori chini ya maji linaendelea muda huu....
No comments