Header Ads

Header ADS

Njombe:Basi la abiri latumbukia mtoni



Watu 13 wamenusurika kifo baada ya basi la abiri lenye namba za usajili T 802 DEZ kampuni ya Dosmeza linalofanya safari zake Njombe-Iringa kuacha njia na kutumbukia mto Ichunilo June 11,2020 majira ya saa moja na dakika hamsini,baada ya kumaliza mteremko mkali wa Ruhuji mjini Njombe. 

Akizungumza mara baada ya kupokea majeruhi wa ajali,Mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Njombe (Kibena) Dkt,Alto Damas Mtega,amesema walipokea majeruhi 13 na kuwapa huduma ya kwanza. 

“Tulifanikiwa kuwapokea majeruhi wote na kuwapa hduma ya kwanza na kuwapa matibabu na majeruhi 3 tuliwaruhusu usiku ule ule kwasababu hali zao hazikuwa mbaya,majeruhi wengine 10 tunao wodini bado wanaendelea na huduma za matibabu,katika hao mmoja hali yake sio nzuri lakini matarajio yetu ataendelea kuwa vizuri”alisema Alto Mtega 

Nuhu George na Kissa Mwaisongole,ni majeruhi katika ajali hiyo wanasema walitembea salama kutoka Iringa na dereva wa gali hiyo alikuwa ni mwaminifu lakini tatizo ni kufeli breki katika mteremko huo. 

“Dereva wetu alikuwa mwaminifu na alijitahidi ili kuokoa roho zetu na tulitembea salama mpaka kufika hapa gari ikakosa breki ikaluka na ikaingia kwenye maji”alisema Kissa Mwaisongole 

Aidha kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema basi hilo limepata ajali katika mteremko mkali kutokana na kushindwa kukata kona kwasababu ya mwendo kasi. 

“Basi hili halikuweza kukata kona kama ilivyo ina maana limekuja na mwendo ambao ni kasi,sasa kitakachofanyika hapa ni kuchunguza kama wakati linashuka lilikuwa mwendokasi ama kuangalia Mechanical diffect,na uchunguzi utakapokamilika sheria itafuata mkondo wake”alisema Hamis Issa 

Hata hivyo kamanda ametoa wito kwa madereva wote kuchukuwa tahadhari kubwa wanapoingia mji wa Njombe mara baada ya kufika katika mteremko huo. 

“Enyi madereva wengine kutoka mikoa mingine,hali ya barabara mkoa wa Njombe ni milima na kona kali chukueni tahadhar mnaopo kuja huku hakikisheni magari yana breki za kutosha na muendeshe kwa tahadhari kubwa tuepukane na madhara kama haya yanayotokea”aliongeza kamanda.

 


No comments

Powered by Blogger.