Mfahamu Mtu Mwenye Tattoo Nyingi Duniani
Lucky Diamond Rich (49), ndiye mtu mwenye michoro (Tattoo) mingi mwilini mwake kwa rekodi ya mwaka 2019
-
Mbali na michoro aliyonayo, pia ametoboa masikio na kuyavuta (kama Wamasai), na meno yake ameweka madini ya fedha (Silver), pia amejitoboa sehemu kadhaa za mwili wake
-
Alianza kujiweka michoro mwilini mwake akiwa na umri wa miaka 16, kwa kuwa kazi yake ni maonyesho aliendelea kujichora hadi akawa mtu anayeshikilia rekodi ya kuwa na michoro mingi
-
Alimaliza kujichora mwili wake akiwa na umri wa miaka 28 na akaanza kuboresha michoro aliyo nayo
-
Lucky hajajiweka michoro mipya kwa takriban miaka 6 na bado hakuna aliyekuja kuvunja rekodi yake
No comments