Nape "Mimi Nafanya Vikao Jimboni Kwangu Mtama"
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema yeye anafanya vikao jimboni kwake.
“Mie sio waziri wa Mambo ya Ndani wala jeshi la polisi mie sio msemaji wao. Lakini mimi nafanya vikao jimboni kwangu Mtama,” Nape aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter akimjibu Simon Chimbo.
Chimbo alihoji iweje kuna mambo ambayo hayaekeweki kuna wengine wanaruhusiwa na wengine wanakatazwa.
Aliandika ujumbe huu “Kaka Nape kwanini kuna double standard kiwango hiki? Huku tunaruhusiwa, kule wanakatazwa? Kwanini kusiwe na fair ground kwa vyama vyote?,” alihoji
Kaka Nape, kwanini kuna double standard kiwango hiki?? Huku tunaruhusiwa, kule wanakamatwa?? Kwann kusiwe na fair ground kwa vyama vyote?? https://t.co/iCYO5bW8V4
— Simon Chimbo (@chimbo008) June 24, 2020
No comments