Nandy Afunguka Kumkwapulia Wema Sepetu Bwana
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amesema kuwa hajawahi kugombana na msanii mwenzake Wema Sepetu na wala hajawahi kumchukulia bwana kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiongea.
Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili, mrembo huyo alieleza kwamba kipindi cha nyuma, kuna maneno mengi yalisambaa mitandaoni kwamba yeye na Wema ni kama chui na paka kutokana na kile kilichodaiwa kuwa wameibiana mabwana, jambo ambalo halina ukweli.
“Huwezi amini, mimi na Wema hatujawahi kugombana kabisa, nilikuwa nashangaa wanavyosema eti nilimuibia danga lake kitu ambacho hakina ukweli wowote, siwezi kufanya hivyo halafu kwa nini tuibiane?
Kwani wanaume wameisha hapa mjini? Watu huwa wanaongea sana halafu wanaongea mambo wasiyokuwa na uhakika nayo, nampenda Wema na sitaacha kufanya hivyo, zaidi tunasapotiana sana kwenye kazi,” alisema Nandy.
Stori: Memorise Richard
No comments