Header Ads

Header ADS

Mtangazaji B Dozen Apokewa Rasmi Kwa Shangwe EFM Radio....Apewa Gari Kali Aina ya Benz


Utambulisho wa nyota Cristiano Ronaldo ndani ya Klabu ya Real Madrid ulihudhuriwa na watazamaji 80,000 katika dimba la Santiago Bernabèu, kwa heshima hiyo aliwapa mafanikio makubwa ikiwemo mataji manne ya Ubingwa wa Ulaya na mabao 311.

Jana Mtangazaji B Dozen ametambulishwa rasmi kwenye ofisi za E-FM na TV-E mbele ya Wafanyakazi ambao imani zao kwake zinazidi idadi ya macho 80,000 ya wale waliofika Bernabèu.

Akizungushwa katika idara zote za kampuni hiyo, Dozen alipokelewa kwa furaha na shangwe toka kwa Wafanyakazi wa ngazi zote akiwemo mwanzilishi na CEO @majizzo

B Dozen Amesema katika maamuzi magumu aliyowahi kuyafanya basi hilo la kuhamia EFM kutoka Clouds ni namba moja, pia amesema wale wanaozania amefeli basi tumpe mwaka mmoja hapo EFM alafu ndo waseme kama amefeli ama la...

Inasemekana pia Mtangazaji huyo amekabithiwa gari kali aina ya Benz kama dhawadi yake kukubali usajili wa EFM...

Kikubwa alichoahidi ni kutoa alichonacho na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na timu nzima, lakini pia kujifunza mengi toka kwa kila mmoja ili kwa pamoja kuipa kampuni yao mafanikio zaidi ya yale mataji na mabao ya CR7 pale Los Blancos.

No comments

Powered by Blogger.