Mfahamu Mmarekani Seneta Ernie Chambers Aliyemburuza Mungu Mahakamani
Seneta Ernie Chambers wa jimbo la Nebraska, Marekani mwaka 2008 alimshitaki Mungu akiiomba Mahakama itoe zuio la kudumu dhidi ya Mungu kufanya shughuli zake zenye madhara kama mafuriko, matetemeko ya ardhi, vimbunga, tufani na majanga mengine
-
Inadaiwa katika shauri hilo watu wengi wamekuwa wakijitambulisha kama Mawakala wa Mungu na kufanya mambo mengi maovu lakini hata siku moja Mungu hajajitokeza hadharani kuwakana hivyo wanafanya yote kwa niaba yake na jina lake
-
Mahakama ilimtaka Seneta Chambers kuhakikisha anamtaarifu Mungu kuhusu uwepo wa shauri hilo dhidi yake Mahakamani hapo kwa kumtumia nyaraka zote za kesi kupitia anuani rasmi ya Mungu ili aweze kufika Mahakamani hapo kujibu madai dhidi yake
-
Seneta Chambers aliiambia Mahakama kuwa Mungu yupo kila mahali na anajua kila kitu. Hivyo anajua kuhusu uwepo wa shauri dhidi yake Mahakamani hapo wala hakuna haja ya kumtaarifu labda aamue mwenyewe kutokuja kama ilivyo kwa wadaiwa wengine
-
Seneta Chambers amesema alifungua kesi hiyo ili kukazia vifungu vya Katiba ya Marekani vinavyosema milango ya Mahakama ipo wazi wakati wote kwa mtu yeyote mwenye kuhitaji haki yake, na kwamba mtu yeyote anaweza kumshitaki mtu yeyote
No comments