Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo Mikononi mwa Takururu
Mrisho Gambo aliyetenguliwa kwenye nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, anahojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) akituhumiwa kugawa rushwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Arusha wanaohusika kupitisha jina la mgombea Ubunge
Inelezwa kuwa kwa muda mrefu Gambo amekuwa na matamanio ya kuwania Ubunge jijini Arusha, akiwa anapambana kuhakikisha jimbo la sasa la Arusha linagawanywa na kuwa majimbo mawili
Juni 19, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Gambo na wenzake wawili, Gabriel Daqaro, na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. Maulid Madeni na kugusia sababu za kuondolewa kwa viongozi hao ni kutokuelewana
Jimbo la Arusha linaongozwa na Mbunge wa CHADEMA, Godbless Lema kwa miaka 10 sasa
No comments