Mchungaji Msigwa: Aliyesema CHADEMA hakuna Demokrasia ni Muongo
Mbunge wa Iringa Mjini kupitia CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa, amesema kuwa mtu aliyesema kwamba chama hicho hakina demokrasia ni muongo kwa kuwa hata kwenye mchakato wa Urais, kimetoa nafasi kwa wanachama wake kuwasilisha barua za kutia nia ya kugombea nafasi hiyo.
Msigwa amesema kuwa chama chao kinayo demokrasia na ndiyo maana hata yeye amepeleka barua ya kutia nia ya kugombea nafasi ya Urais.
"Huyo anayesema ndani ya CHADEMA hakuna demokrasia kwani ni lini chama kimetangaza mchakato wa Urais, chama kimetangaza na kimetoa taarifa wazi na ndiyo maana mimi nimepeleka barua, anayesema hakuna demokrasia alikuwa ni mtabiri muongo, kwanza Sumayae hayuko kwenye chama chetu" amesema Msigwa.
Juni 4, 2020, Msigwa alipeleka barua yake ya kutia nia ya kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu ujao.
No comments