Mbunge David Silinde Atangaza Kujiunga CCM Baada ya Kuvuliwa Uanachama Chadema
Mbunge wa Jimbo la Momba, Mkoani Songwe David Ernest Silinde ametangaza kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mbunge huyo pamoja na Anthony Komu, Joseph Selasini na Wilfred Lwakatare walifutwa uanachama na CHADEMA kwa kile kilichoelezwa ni kukiuka maagizo ya chama
Kabla ya kufutwa uanachama, alijiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA mwezi Mei, baada ya Wabunge wenzake kumtaka kufanya hivyo kwa kutotii agizo la kutokwenda Bungeni
Wakati anajiuzulu alisema wananchi ndiyo walimtuma Bungeni, hivyo hata akikosa udhamini wa CHADEMA, atatumia chama kingine
No comments