Header Ads

Header ADS

Marekani yataka Uchunguzi juu ya Shambulio la Mbowe Ufanyike



Ubalozi wa Marekani umesema kwamba tukio hilo ni la kikatili na lisilo la sababu .

Ubalozi huo umesema kwamba umesjhtushwa na tukio hilo na kutoa pole kwa mbunge huyo na familia yake.

''Ubalozi wa Marekani umeshtushwa na kuhuzunishwa na tukio la kikatili la kushambuliwa kwa mbunge na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tarehe 9 Juni, tunatoa pole kwa mbunge huyo na familia yake'',ilisema taarifa hiyo.

Ubalozi huo umelitaja shambulio la kiongozi huyo wa Chadema miongoni mwa mlolongo mrefu wa matukio ya kusikitisha ya utumiaji wa nguvu na unyanyasaji yanayofanywa dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani.

Aidha ubalozi huo umetambua kwamba mojawapo ya mashambulio hayo ya kikatili dhidi ya viongozi wa upinzani ni jaribio la mauaji lililotokea tarehe 7 mwezi Septemba 2017 dhidi ya Tundu Lissu ambalo ufumbuzi wake haujapatikana hadi leo.

No comments

Powered by Blogger.