Header Ads

Header ADS

Majibu Feki ya Corona yagundulika Uganda


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuna uzembe umefanyika Maabara na kupelekea Watu kuambiwa wana corona wakati hawana

 “tuna maambukizi 679 ya corona hadi sasa Uganda ila kati ya hawa Watu baadhi yao wameambiwa wana corona baada ya vipimo vya Maabara pale Makerere wakati hawana, Maabara imekosa umakini, inaonekana kuna wafanyakazi wachache Maabara na huenda walichoka”

Museveni anatoa kauli hii ukiwa umepita mwezi mmoja tangu Rais Magufuli aliposema vipimo vya maabara ya corona vina shida na kupelekea kuundwa kwa Tume ya uchunguzi ambayo ilithibitisha kauli ya JPM na hatua kuchukuliwa ikiwemo kuanza kutumika kwa Mabaara mpya, JPM alitoa kauli hiyo akiwa Chato May 03,2020 .

Rais Magufuli alisema "Kama tunapeleka Sampuli za wanyama bila wao kujua na zinakuwa positive inawezekana wafanyakazi wa Maabara wanatumika na Mabeberu, Kama mapapai, mbuzi wana corona, basi WHO wanapaswa kufanya kazi kubwa ya ziada, kwa hili lililotokea lazima Kuna watu wameambiwa wana corona wakati hawana"


No comments

Powered by Blogger.