Header Ads

Header ADS

Lema Afunguka "Madini ya Tanzanite Yameuzwa Kama Wanauza saa ya Mike Tyson kwa Kukosa Uelewa"



Aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema kukosekana uelewa wameshusha thamani ya Tanzanite kwa hali ya juu.

“Piece ya kilo 9.27 na 5.28 ni unique pieces ambazo kwa bei mnayo pigia kelele sio zaidi ya USD 3.5 milioni,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa twitter.

“Najiuliza sasa ni pieces gani nyingine zitapata thamani kuonyesha upekee wa madini haya,” aliandika Lema.

Lema  amesema madini hayo ambayo ni adimu bei zake hazipangwi kwa gramu isipokuwa upekee.

“Kuna rules katika biashara hizi, rules hizo hazihitaji degree/PHD isipokuwa wall street thinking. Nani ataona thamani ya Tanzanite kwa kilo 9.27/5.28 kuuzwa sawa na saa ya Mike Tyson na mnunuzi ni serikali?,” aliandika Lema.


No comments

Powered by Blogger.