Kukonyeza Aina Mpya Ya Ukatili kwa Wanawake wa Dar
Afisa ustawi jamii kwenye hospitali ya Amana Suphian Mndolwa amesema vitendo vya ukatili wa kingono kwa wanawake jiji la Dar es salaam vimezidi kukithiri kwa siku za hivi karibuni.
Akizungumza na televisheni mtandao ya Daily news digital Mndolwa amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kingono wa aibu vimezidi kwa wanawake na serikali inapaswa kutoa elimu kwa wanawake ili waweze kuripoti vitendo hivyo.
“Kuna aina mbili za ukatili kuna ukatili wa kushika na ukatili wa aibu, ukatili wa aibu kwa wanawake mfano kumpiga kope mwanamke (kukonyeza) ni ukatili maana una muathiri kisaikolojia, kwa sasa hivi vitendo hivi hapa Dar es salaam vimekithiri sana hasa kwa wanawake wenye maumbile makubwa wanapotembea mitaani” amesema.
“Kwa sasa tuneshafungua mafaili mengi Ya kesi za aina hii lakini inapasa watu wapewe elimu ili waweze kuripoti matukio haya” ameongeza.
No comments