Header Ads

Header ADS

Lavalava Amka, Hatukuoni Ukitusua nje ya WCB



Ada ya mja hunena, muungwana ni vitendo

Sikia hii, labda kama umezaliwa kuishi na kufa (kimziki) ndani ya WCB. Pengine unalijua hili, na huna cha kufanya kwa maana uwezo wako ndo umeishia hapo.

Madogo wanakuja, madogo wanakua na wanaondoka. Huoneshi kujitanua, ulisikika vema ulipoingia lakini sasa hali ni mbaya.

Usije kusema hujaambiwa, kama kuna wanaokusifia kuwa bado ni mkali basi ujue wanakulamba kisogo. Labda kama una ‘ukali’ mwingine unaokutetea na kukuongezea mbeleko

Niliwahi kuwa shabiki yako, nyimbo zako kadhaa ziliwahi kunirahisishia ‘kazi’ mahali fulani. Nalazimika kuendelea kukukubali kama sehemu ya fadhila, ila usipoamka utaona vumbi tu

Siku ukifurushwa hapo ndo akili zitakukaa sawa, kama ni uwezo umegota bora ukimbie kwa visingizio kama yule mwingine kabla ya fedheha ambayo hutoweza kujitetea

Ukibebwa, jishikie

No comments

Powered by Blogger.