John Heche Acharuka "Tunakoelekea Tunaweza Kuwakosa Wasanii na Sanaa ikafa"
Aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amesema wanakoelekea wanaweza kukoss wasanii na sanaa ikafa.
Heche aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter kuwa lengo la kueleza ni kwa sababu kila msanii atakuwa Mbunge.
“Huko tunakokwenda tunaweza kukosa wasanii na sanaa ikafa kwa sababu kila msanii atakua Mbunge,” aliandika Heche.
Hivi karibuni wasanii mbalimbali wamejitokeza na kueleza kuwa wana nia ya kugombea ubunge.
Jana Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa bongo Flavor Joachim Kimaryo maarufu kwa jina la Master J ametangaza nia kugombea ubunge kwenye jimbo la Rombo kwenye uchaguzi.
Huko tunakokwenda tunaweza kukosa wasanii na sanaa ikafa kwasababu kila msanii atakua mbunge.— John Heche (@HecheJohn) June 25, 2020
No comments