Header Ads

Header ADS

Grealish na Havertz Wavutana Manchester United


Manchester United wamenuia kumsajili nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, msimu huu lakini wanaweza kubadilisha mpango huo kama Kai Havertz 20, wa Bayer Leverkusen atawekwa sokoni.H

Hata hivyo Bayern Munich wanaamini wataweza kumshawishi mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz 20, na kuipiku Manchester United.
Leicester City hawana hofu ya kumpoteza mlinzi wa pembeni Ben Chilwell kwa sababu wanaamini wakifuzu michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya itakuwa njia pekee ya kumbakiza beki huyo.
Mbweha hao wanatahitaji £60m kwa kitasa hicho chenye miaka 23 kwa timu yoyote itakayohitaji huduma yake.

Liverpool watajaribu kumshawishi winga wa Borrusia Dortmund Jadon Sancho 20, na kuzipiku Real Madrid na Manchester United.
Winga wa Manchester City Leroy Sane, 24, ataingia kandarasi ya miaka mitano na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Bundesliga Bayern Munich baada ya kuwa katika hatua nzuri ya kukamilisha uhamisho wake.

Everton wamepanga kumsaini mlinzi wa Paris Saint Germain na Brazil Thiago Silva, ambapo mkataba wa beki huyo unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni, AC Milan pia inawinda saini ya Silva, 35.

Arsenal huenda ikamsajili mlinzi wa kulia wa Norwich City Max Aarons, 20, baada ya kuvutiwa na kiwango chake ingawa hawako tayari kumchukua kwa dau la pauni milioni 30 ambazo Norwich wanahitaji.

Manchester City wako katika mchakato wa kumchukua mlinzi wa Barcelona Sergio Roberto ingawa dili hilo litafanikiwa tu endapo Barca watamruhusu kuondoka klabuni hapo.

No comments

Powered by Blogger.