Header Ads

Header ADS

DC Jokate Amlilia Shamsa Mke wa Babu Tale..."Alinitimia Ujumbe Nimlelee Wanawe"



"Shammy tarehe 11.06.2020 ulinitumia huu ujumbe wa simu- Buriani. Nilelee wanangu! Nilishtuka kupata huu ujumbe kutoka kwako. Sikuelewa. .
.
Leo bado sielewi. Ila nitajitahidi kufanya kama ulivyoniomba. Nilikupenda, nilikuheshimu kwasababu ulikuwe mtu mwema sana na muungwana sana na ndio maana ulipo sema unafunga safari kuja Kisarawe kuniona nikakuandalia na chakula maalum kama mgeni wangu maalum.

Nilikuambia kipindi kile na ninasema tena leo unepoelekea kuwekwa kwenye nyumba yako ya milele. Sijawahi kutana na dada kama wewe, uliyejaa upendo, ucheshi, uvumilivu, utulivu na akili. Na kila siku nilikuwa namwambia @babutale katika vitu inafaa amshukuru sana Mungu ni kukupata wewe kama mke na mama wa watoto wake. Licha ya urembo na umaarufu ulikuwa na busara na utulivu sana. Upumzike kwa amani my dear Shammy ❤️BY @jokatemwegelo

No comments

Powered by Blogger.