Aston Villa yabanwa mbavu na Newcastle
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza muda wote, Aston Villa ikitoa sare ya 1-1 na Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. James’ Park.
Wenyeji, Newcastle United walitangulia kwa bao la Dwight Gayle dakika ya 68 kabla ya Ahmed Elmohamady kuisawazishia Newcastle United dakika ya 83.
Kwa sare hiyo, Aston Villa inafikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya 19 mbele ya Norwich City yenye pointi 21 za mechi 31, ikizidiwa wastani wa mabao na West Ham United na AFC Bournemouth.
Liverpool inaendelea kuongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi zake 86 baada ya kucheza mechi 31, ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 63 za mechi 30, Leicester City pointi 55 mechi 31, Chelsea pointi 51 mechi 30 na Manchester United pointi 49 mechi 31.
Kikosi cha Newcastle United kilikuwa: Dubravka, Manquillo, Lascelles, Fernandez, Rose, Ritchie/Gayle dk67, Shelvey, Hayden/Bentaleb dk86, Saint-Maximin, Almiron/Lazaro dk86 na Joelinton/Carroll dk64.
Aston Villa: Nyland, Konsa/Elmohamady dk77, Hause, Mings, Targett, McGinn/Nakamba dk77, Douglas Luiz, Grealish, El Ghazi/Hourihane dk70, Samatta na Trezeguet/Davis dk70.
No comments