Watetezi wa Haki za Binadamu Walaani Cecil Mwambe Kurejea Bungeni...Kumburuza Spika Kortini
Shirika la Elimu ya Uraia na Msaada wa Sheria (CiLAO) limeeleza kusikitishwa na kitendo cha Spika wa Bunge la Tanzania kufanya maamuzi yanayoelezwa kukiuka misingi ya Katiba ya Tanzania
Kitendo walichokisikitikia na kukilaani ni cha Spika Job Ndugai kumruhusu aliyekuwa Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe ambaye alijiuzulu nafasi yake ya Ubunge aendelee na kazi hiyo
CiLAO imesema kwa mujibu wa Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ni wazi kuwa Mbunge atapoteza nafasi yake ya ubunge ikiwa atapoteza uanachama wa chama chake kilichompatia ubunge wakati wa uchaguzi
Mwambe alionekana akitangaza kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na CCM. Mkurugenzi wa CiLAO, Odero Odero amesema "Kwa kuwa Mwambe alitangaza kijiondoa CHADEMA tunaamini pasipo shaka alipoteza sifa ya kuwa Mbunge wa Bunge la Tanzania"
Shirika hilo kwa kushirikiana na Wadau wengine limeazimia kwenda Mahakama Kuu haraka iwezekanavyo kufungua kesi kuomba ufafanuzi wa Mahakama kuhusu kitendo hicho cha Spika
No comments