Viongozi wa Afrika Mashariki inabidi Mkubali Tanzania Bado ni Nchi Tegemeo Kwenu
Nikirudi kwenye mada inayo sema viongozi wote wa nchi za East Africa mkubali kwamba Tanzania ni nch tegemezi kwenu na kiongozi ambae bado mnahitaji uongozi wake ili tuweze kufika tunapostahili kama wanaAfrika Mashariki.
Nimesema bado Tanzania ni kiongozi bora na ataendelea kuwa Bora kama alivyokuwa zamani enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika harakati za kuhakikisha East Africa inasimama imara kiuchumi kimuongoza hata kifikra
Tanzania tulikuwa nchi ya Kwanza kuonesha umoja wetu pale tulipohitajika kutoa msaada na Sio East Africa tu Bali na nch nyingine nyingi tulisaidia kwa na tulitoka kwa mafanikio makubwa kwani TANZANIA haikuwa na historia ya kushindwa
Na ndio maana hata kwenye Corona tutashinda sababu nchi yetu imejengwa katika misingi imara. Tanzania imeendelea kuwa mkubwa na msimamizi mzuri siku zote nina imani viongozi wa East Africa walitakiwa baada ya janga ili la Corona kuzikumba nchi zetu wangejaribu kuuliza kwanza kwa kiongozi wao TANZANIA wafanye nini au wachukue hatua gani nina imani wangepata njia inayostahili kuliko kufuata njia ambayo imepelekea wananchi kuzichukia Serikali zao uchumi wa nchi kushuka. Kitu ambacho kinaenda kuwafanya warudi kwenye maisha yao ya kawaida huku wakitegemea mikopo kwa asilimia kubwa kitu ambacho kitafanya nch ni zao lakini waendelee kutawaliwa
Uganda Rwanda, Kenya, Congo hawakupaswa kufungia watu ndani walipaswa wamsikilize kiongozi wao juu ya kufungia watu ndani na athari za uchumi wa Serikali na hata wananchi wenyewe. Leo Uingereza imetangaza Jumatano itafungua nchi na watu warudi wakaendelee na majukumu yao ili hali bado ugonjwa upo na vifo vipo kwa wingi. Je, viongozi wa East Africa waliopo majirani wameshindwa kuona kuwa Magufuli anaposema tusifungie watu ndani tukachape kazi ni muhimu wanasubiri mpaka mzungu ambae yuko mbali nao kaona Magufuli ni kiongozi wa kuigwa na tayari ameshafuata njia zake kama kiongozi mwenye busara pia mpaka sasa anatumia msemo wake wa tutoke nyumbani tukafanye kazi Ila chukua tahadhari
Hivi ndugu zangu wa Afrika Mashariki mtawaambia nini wananchi wenu pale mtakapofungua nchi ilihali ugonjwa haujaisha? Vipi wale waliopoteza ndugu zao kwa kupigwa na Askari mpaka kufa vipi wananchi waliowapigia kura mnaenda kuwaruhusu watoke nje baada ya kuwafungia ndani kwa muda na kufanya wengine wale misingi yao je mtawapa mitaji
Vipi wale waandishi wa habari walioandika unanii wa Rais wetu wataficha wapi sura zao kwa aibu baada na wao kuamua kuwa na unanii kama wa Rais a kuachana na umagharibi
Viongozi wetu pendwa wa East Africa bado hamjachelewa pia ili janga la Corona liwe somo kwenu kwamba hata ikija kutokea tena tatizo mkimbilie kwanza kwa wakubwa zenu ili mpate muongozo na ushauri sio kuiga kila kitu kwa mzungu kwani hata sisi viongozi wetu wana busara za uongozi
Pia Sina hakika kama kuna kiongozi wa East Africa alifanya uchunguzi wa vipimo vyake kama Rais Magufuli alivyowashauri kama hawajapima nitajiuliza ni uvivu au wamegoma kutoa Kiki ?
Ila muwe mnaelewa aliyekushinda kakushinda tu hivyo viongozi wa Afrika mjitthmini.
No comments