Mwakyembe "Ligi Kuchezwa Bila Mashabiki"
Serikali kupitia Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dk Harrison Mwakyembe amesema wanaendelea kujadiliana na vyombo vinavyosimamia michezo nchini kuangalia jinsi watakavyoweza kurejesha michezo baada ya tamko la Rais Dk John Magufuli
Akizungumza baada ya kikao alichofanya na wadau, Dk Mwakyembe alisema ameliagiza Baraza la Michezo na Taifa (BMT) na TFF kuangalia jinsi wanavyoweza kuvisaidia vilabu kiuchumi ili kuweza kumudu gharama pale ligi itakaporejea.
“Tumewaagiza BMT na TFF wawasiliane na FIFA, CAF ili kuomba fedha za kusaidia vilabu wakati huu wa changamoto ya Corona”
“Ligi itakaporejea, kwa mechi kuchezwa bila ya mashabiki, timu zitakuwa kwenye wakati mgumu sana, Huu ni wakati ambao vilabu vinapaswa kusaidiwa na vyombo hivi ambavyo tunafahamu vina pesa ya kutosha,” amesema Dk Mwakyembe.
Tayari FIFA imetangaza kutoa mgawo wa zaidi ya Dola Milioni 150 kwa Wanachama wake katika jitihada za kuwasaidia kutimiza majukumu yao wakati huu wa kukabiliana na corona. TFF inatarajiwa kupokea zaidi shilingi bilioni moja kutoka mgawo huo.
No comments