Header Ads

Header ADS

Msanii Jack Wolper Amesema kwa Sasa Ana Wanaume Wanne


Msanii Jack Wolper Amesema kwa Sasa Ana Wanaume Wanne

Msanii wa Filamu nchini, Jacqueliner Wolper, amesema ana wapenzi kama wanne kwa sasa ila anamuangalia mwenye tabia nzuri ndiye atakayemchagua kuwa naye.

“Huwa simuweke mjini mwanaume na sina kashfa  ya kumuweka mwanaume mjini ninajijua mimi ni nzuri, msafi na ninajua kupika siwezi kufanya hivyo,” amesema Wolper

Msanii huyo amesema hana tabia ya kurudiana wala kuzungumza na wanaume zake alioachana nao.

Pia amesema hajawahi kupenda mume wa mtu kwa kuwa ana wivu katika mapenzi na anapenda kuwa na uhuru na mwanaume wake.

“Sina tabia ya kurudiana na wala kuongea na Ex wangu  na sijawahi kupenda mume wa mtu maana mimi nina wivu napenda uhuru wa kuwa na mwanaume wangu,” amesema Wolper

No comments

Powered by Blogger.