Header Ads

Header ADS

Majibu ya Calisah Kuhusu Kusambaza Picha za Utupu


Mwanamitindo na video vixen Calisah amejibu kuhusu picha na video zilizosambaa mitandaoni zikimuonyesha maungo yake yake ya ndani baada ya taulo alilovaa kumdondoka wakati akiinga bafuni.

Akizungumza kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV, Calisah amesema tukio hilo limetokea kwenye mtandao wa Snapchat wakati anaenda kuoga, nia yake ni kumtumia picha mwanamke wake ili kumuaminisha kama kweli anafanya kitendo hicho.

"Majuto ambayo ninayo ni kwa dada yangu au kama ningekuwa na mtoto wa kike ambaye angeiona hii video japo tukio hilo limenitingisha na ni aibu kwa familia yangu, nilikuwa naongea na mwanamke wangu kwenye "face time" nikamwambia acha nikaoge akawa haamini nikamwambia nitakutumia video muda sio mrefu" amesema Calisah

"Sasa mtandao wa Snapchat una sehemu ya kuziweka au kushea ambazo zipo karibu sana, wakati narekodi nilikuwa nataka  niisave na mikono yangu ilikuwa ina maji, kwa bahati nikabonyeza sehemu ya kutuma na kushea ila baadaye nikaifuta" ameongeza

No comments

Powered by Blogger.