Jeshi la Ethiopia Lakiri Kudungua Ndege ya Kenya, Bahati Mbaya
Ethiopia imekiri kuidungua ndege ya Kenya katika anga la Somalia mapema wiki hii na kusabbaisha vifo vya abiria wote watano waliokuwamo kwenye ndege hiyo.
Taarifa ya jeshi la Ethiopia iliyotumwa kwa Umoja wa Afrika (AU), imesema ndege hiyo mali ya kampuni binafsi ya nchini Kenya, iliangushwa siku ya Jumatatu kwenye eneo la kusini magharibi ya Somalia.
Taarifa hiyo imesema wanajeshi waliidungua kwa bahati mbaya baada ya kuamini ndege hiyo ilikuwa kwenye mpango wa kujiripua kwani hawakujulishwa kuhusu safari yake na ilikuwa ikiruka usawa wa chini kuliko kawaida.
Kulingana na taarifa ya jeshi, ndege hiyo ilikuwa imebeba shehena ya bidhaa za matibabu na msaada wa kiutu ikiwa na abiria watatu raia wa Kenya na wengine wawili raia wa Somalia.
Kenya imeelezea kufadhaishwa na mkasa huo ikisema safari ya ndege hiyo ilelenga kuisaidia Somalia kupambana na virusi vya corona.
No comments