Header Ads

Header ADS

Ameandika Roma & Stamina [Rostam] Kuhusu Ventilator Challenge


Ameandika Roma & Stamina [Rostam] Kuhusu Ventilator Challenge

Kwa Jinsi Ambavyo Nimeona Watu Wengi Mmeupokea Wimbo Wetu Wa KAKA_TUCHATI Na Kuvutiwa Nao,

Nimewaza Jambo Fulani, Mimi Nina Followers Hapa Instagram Laki Sita 600K, Na Staminashorwebwenzi Ana Followers Laki Saba 700K

Sisi Ni Wasanii Masikini (Tusio Na Kipato Kikubwa) Lakini Tumejaliwa Vipaji Na Utajiri Wa Watu (Mashabiki)

Tukisema Kati Ya Hao Tuchukue Followers 600K tu, Kama Kila Mmoja Kutokana Na Kuguswa Kwake Na Kuupenda Na Kuufurahia Wimbo Huu KAKA_TUCHATI Nikiomba Achangie Tsh. 500 tu!! (Mia Tano Tu) Kwa Ajili Ya Project Hii, Na Kama Wote Watu Laki Sita Watachangia Basi Itapatikana Tsh 300M (Milioni Mia Tatu).

Mashine Moja Ya Ventilator Gharama Yake Ni Tsh. 100M

Hivyo Basi Tukifanikiwa Kupata Hizo Milioni 300, Tuna Uwezo Wa Kununua Ventilator 3 Na Zitasaidia Kuokoa Maisha Ya Ndugu,Jamaa Na Marafiki Zetu Wengi Kwenye Janga Hili La Corona Covid_19 Hasa Mikoani Ambako Ndio Kuna Uhitaji Zaidi!! .

Lengo Letu Kama #Rostam (Roma Na Stamina) Ni Kusaidia Jamii Yetu Kama Yalivyo Maudhui Ya Nyimbo Zetu Nyingi Na Kuacha Alama Chanya Kupitia Sanaa Tunayoifanya Hasa Kwenye Huu Wimbo Wetu Mpya Wa KaKa_Tuchati Ambao Umetokea Kupokelewa Vizuri Sana!! Tunaamini Mashabiki Zetu Na Hata Wale Wasio Mashabiki Zetu ila Wamependa Tulichokifanya Katika Hili Mna Uwezo Wa KutuSupport Kulifanikisha Hili Zoezi.

Rostam Tunataka Kununua Mashine Ya Ventilator Angalau Hata Moja Na Hii Ndiyo Itakuwa Challenge Ya Wimbo Wetu KaKa_Tuchati

Mashabiki Wa Muziki Na Sanaa Yetu/Viongozi Wa Serikali/Viongozi Wa Dini/Wanasiasa/Wafanyabiashara Na Wajasiriamali/Wanafunzi/WasaniiWenzetu na Wadau/Wanaharakati/MashirikaBinafsi/TaasisiMbaliMbali/KampuniMbaliMbali/ Na Hasa Vyombo Vya Habari Na Yoyote Aliyeguswa Na Hili Ningeomba Tuungane Kwa Pamoja Kulifanikisha Hili Zoezi Na Kuusambaza Ujumbe Huu Wa Hii Challenge Ya Rostam
KaKa_Tuchati Ventilator_Challenge .

Na Tuisaidie Jamii Yetu Katika Hili La Kuokoa Roho Za Ndugu Zetu Kwenye Janga Hili La Corona!! .

NB - Hata Ukiwa Na Kiasi Pungufu Na Tsh 500 Utakuwa Umechangia Pia Na Tutapokea Na Kukushukuru, Na Hata Ukiwa Una Kiasi Cha Zaidi Ya Tsh 500 Tutashukuru Na Utakuwa Umechangia Pakubwa Zaidi.

No comments

Powered by Blogger.