Header Ads

Header ADS

Swala Roma Mkatoliki Kusemekana Katorokea Marekani Latua Bungeni...Waziri Afunguka


Utamaduni sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe asema msanii wa muziki wa kizazi kipya Roma Mkatoliki hajatoroka nchi kutokana na serikali kandamizi

Ajibu swali la Mbunge wa viti maalum kwa Devotha Minja, Waziri Mwakyembe amesema wanasiasa wa upinzani wanawajaza maneno yasiyo na uhakika wala ukweli wowote wananchi na vijana wanaofanya jitihada za kutafuta kipato

“..Mimi nataka mheshimiwa aniletee ushahidi kwamba Roma amekwenda Marekani kwa sababu ya serikali kandamizi Hapana Roma amekwenda kwa hiari yake mwenyewe na mimi nimeongea naye alitaka kurejea nchini lakini hili swala la corona ndo limemkwamisha kurejea ..kama anaweza akodi ndege ya pekee yake arejee nchini” Mwakyembe

Baadhi ya Picha: Roma Mkatoliki na Waziri Mwakyembe walivyokutana ...
Roma kabla ya kwenda nchini Marekani aliwahi kutekwa na watu wasio julikana lakini alirejea uraiani baada ya kukutwa akiwa ametelekezwa na watekaji hao baada ya siku takribani 3





No comments

Powered by Blogger.