Nahodha Yanga: Ligi Irudi, Tumemisi Utamu Wa Morrison
JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga, amesema kuwa anaomba dua usiku na mchana janga la Virusi vya Corona lipite ili ligi irejee kutokana na kukumbuka madude ya kiungo wao, Bernard Morrison.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Abdul alisema kuwa kwa sasa wamekuwa wanyonge nyumbani kutokana na kushindwa kuendelea kucheza baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa na serikali.
“Kuna mambo mengi ambayo nimekumbuka ndani ya ligi ikiwa na madude ya Morrison ukiachana na hayo pia namna mashabiki ambavyo walikuwa wanatupa sapoti ilikuwa ni raha.
“Muda mwingi kwa sasa ninautumia nikiwa nyumbani na mazoezi ninafanya bila uwepo wa kocha, ni balaa tupu yaani ninapenda hali irejee kama zamani maisha yaendelee,” alisema Abdul.
Wakati ligi ikisimam-ishwa Abdul alihusika kwenye mabao matano kati ya 31 yaliyo-fungwa na Yanga ambapo alitoa pasi tano za mabao.
Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam
No comments