Kwa mujibu wa WHO hizi dawa tatu ndio zenye matumaini makubwa ya kutibu Corona, Ikiwemo ARVs
Zaidi ya wa watu 150,000 wamefariki kutokana na virusi vya Covid 19 , lakini kufikia sasa hakuna dawa zilizothibitishwa kutibu ugonjwa huo. Zaidi ya dawa 150 zinafanyiwa utafiti duniani.
Nyingi kati ya yazo ni dawa zilizopo ambazo zimekuwa zikifanyiwa majaribio dhidi ya virusi hivyo.
Shirika la Afya Duniani WHO limezindua majaribio ya pamoja ili kuchunguza tiba yenye matumaini.
Uingereza inasema kwamba majaribio yake ndio makubwa zaidi dunuiani huku zaidi ya wagonjwa 5000 wakishiriki.
Na vituo vingi vya utafiti duniani vinajaribu kutumia damu ya waliopona kama dawa.
kuna aina tatu ya dawa zinazochunguzwa:
Dawa za kukabiliana na virusi vya ukimwi ambazo zinaathiri moja kwa moja uwezo wa virusi kushamiri mwilini zinaweza kuisaidia kinga – wagonjwa huathirika zaidi kinga zao zinapofanya kazi ya ziada na kusababisha uharibifu mwilini.
Lakini ni dawa gani yenye matumaini ya kuzuia virusi vya corona?
Dkt Bruce Aylward, kutoka kwa shirika la Afya duniani , alisema kwamba Remdesivir ndio dawa ya pekee inayoonyesha ishara za matumaini, baada ya kutumika China.
Unachohitajika kufanya ili kuzia mambukizi ya virusi hivi
Dawa hiyo ya kukabiliana na virusi ilitenegenezwa kutibu Ebola lakini pia ikaonyesha kwamba inaweza kutibu magonjwa mengine.
Imeonekana kufaulu kutibu magonjwa mengine hatari ya coronavirus kama vile MERS na matatizo ya mapafu katika utafiti uliofanyiwa wanyama , ikionyesha matumaini ya uwezo wa kutibu virusi vya corona.
Matokeo ya majaribio ya dawa hiyo yaliovuja yalionyesha kwamba ina uwezo.
Ni mojawapo ya dawa nne katika majaribio hayo ya pamoja yanayofanywa na WHO huku kampuni inayoitenegeneza dawa hiyo Gilead pia ikiandaa majaribio.
Kumekuwa na mazungumzo chungu nzima , lakini yenye ushahidi mchache kwamba dawa tofauti za kukabiliana na virusi vya corona Loponavir na ritonavir zinaweza kutibu virusi vya corona.
Kumekuwa na ushahidi kwamba zinaweza kufanya kazi katika maabara lakini utafiti miongoni mwa watu hazina matokeo ya haja.
Mchanganyikio wa dawa hizo mbili haukuimarisha hali ya mgonjwa kupona, kupunguza viwango vya vifo ama hata kiwango cha virusi kwa mgonjwa mwenye Covid 19.
Hatahivyo,huku majaribio hayo yakifanyiwa wagonjwa walio katika hali mbaya zaidi, karibia robo yao walifariki ikimaanisha kwamba huenda dawa hizo haziwezi kufanya kazi iwapo mgonjwa yuko katika awamu za mwisho za virusi vya corona.
Je dawa za malaria zinaweza kuzuia virusi vya corona?
Dawa za kukabiliana na malaria ni miongoni mwa dawa zinazofanyiwa majaribio na WHO.
Chloroquine na Hudroxychloroquine zinaweza kuwa na uwezo wa kukabiliana na virusi vya corona mbali na kuzuia kinga kushambuliwa na virusi hivyo.
Dawa hizo zimeongezawa umaarufu kama mojawapo ya tiba za coronavirus, kutokana na madai yaliotolewa na rais Trump , lakini pia kuna ushaidi mdogo kuhusu uwezo wake.
Hydroxychloroquine pia hutumika kama tiba ya ugonjwa wa baridi yabisi kwa kuwa inaweza kusaidia kinga mwilini.
Majaribio katika maabara yameonyesha kwamba inaweza kuzuia virusi hivyo na kuna ushaihidi kutoka kwa madaktari unaosema inaweza kuwasaidia wagonjwa.
Hatahivyo, WHO inasema kwamba hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuhusu uwezo wake.
Je dawa za kujenga kinga mwilini?
Iwapo kinga mwilini inakabiliana na virusi basi inaweza kusababisha uvimbe mwilini.
Hii hutokea iwapo mfumo wa kinga umepewa jukumu la kukabiliana na maambukizi , lakini hali hiyo inaweza kusababisha uharibifu mwilini na kusababisha kifo.
Majaribio hayo ya pamoja yanayofanywa na WHO pia yamehusisha dawa ya interferon Beta , ambayo hutumika kutibu mzio na uvimbe mdogo.
Interferon ni kundi la kemikali zinazotolewa mwilini wakati kinga inaposhambuliwa na virusi.
Je damu ya waliopona Covid 19 inaweza kutibu corona?
Watu waliopona maambukizi ya virusi vya corona wanapaswa kuwa na antibodies katika damu zao ambazo zinaweza kushambulia virusi hivyo.
Wazo ni kuchukua sehemu ilio na antibodies hizo katika damu na kumpatia mgonjwa kama tiba.
Marekani imefanikiwa kutibu wagonjwa 500 kwa kutumia plasma hiyo na mataifa mengine yameanza kufuata mkondo huo.
Je itachukua muda gani kabla ya tiba kupatikana?
Ni mapema mno kujua ni lini tunaweza kupata dawa ya kutibu virusi vya corona.
Hatahivyo , tunapaswa kuanza kupata matokeo ya majaribio katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Hiyo ni mapema zaidi ya tutakavyojua iwapo chanjo inayolinda dhidi ya maambukizi badala ya kutibu ina uwezo.
Hiyo ni kwa sababu madaktari wanajaribu dawa ambazo tayari zimetenegenezwa na zinajulikana kuwa salama katika upande wa matumizi yake , huku watafiti wa chanjo wakilazimika kuanza mwanzo.
Viliveile kuna dawa mpya za kukabiliana na virusi vya corona ambazo zinafanyiwa majaribio katika maabara lakini haziko tayari kufanyiwa majaribio miongoni mwa wanadamu.
Kwa nini tunahitaji tiba?
Sababu ya wazi ya kutaka tiba ni kwamba itaokoa maisha, lakini pia inaweza kufutilia mbali amri za kutotoka nje.
Tiba yenye uwezo itafanya virusi vya corona kukosa nguvu.
Iwapo itazuia watu waliopo hospitali kuhitaji mashine za kusaidia kupumua basi hakuttakuwa na haja ya wagonjwa kupelekewa katika vyumba vya wagonjwa mahututi hivyobasi hakutahitaji uangalizi wa makini wa wagonjwa.
No comments