Header Ads

Header ADS

Dk Mwigulu Amcharua Zitto Kabwe Amemuambia kwani Rais ni Nesi Umuone Anapokea Wagonjwa?


Mbunge wa Iramba (CCM), Dk. Mwigulu Nchemba, amemtolea povu kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya kudai Rais amekwenda kujificha Chato.

Nchemba amemuambi Zitto kuwa Rais sio nesi iwe ni lazima amuone anapokea wagonjwa ndio ajue yuko ofisini.

“Serikali iko kazini kila huduma wanayopata wagonjwa maana yake Rais yupo kazini,” aliandika Nchemba katika ukurasa wake wa Twitter huku akimjibu Zitto alichokuwa amekiandika.

Nchemba aliendelea kumuambi Zitto kuwa amekimbia bunge badala ya kuwa pamoja na kushauriana kwa njia sahihi ya bungeni amejificha.

“Zitto umekimbia bunge badala uje tuishauri serikali kwa platform sahihi bungeni, umejificha, umebaki insta,”


No comments

Powered by Blogger.