Vanessa Awaziba Midomo Wanaomsengenya
BAADA ya habari kusambaa kuwa tangu aingie kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Marekani, Rotimi amesahau kufanya kazi. Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amewaziba midomo wanaomsema na kuwaambia kuwa, kula kwake bata na mpenzi wake, hakumzuii kufanya kazi.
Akipiga stori na Amani, Vanessa alisema watu wanaongea sana kuwa kwa sasa hafanyi kazi, muda mwingi anaonekana akila bata na mpenzi wake, jambo ambalo siyo kweli kwani kuna kazi kibao zinakuja.
“Watu wamezoea sana kuongea, kuzunguka kwangu kula bata na mpenzi wangu hakumaanishi kuwa sifanyi kazi bali niwaambie tu kwamba muda mwingi Rotimi ananisapoti katika kazi yangu yaani muda wa kazi ukifika nafanya. Nasubiri kipindi hiki cha corona kiishe, ndipo watu wataona kazi zangu kibao,” alisema Vanessa.
No comments