Profesa Jay: Kuna Watu Wanafanya Figisu ili Kutukwamisha katika Uchangiaji wa Fedha kwa viongozi Wetu Waliopo Segerea
Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa Jay amesema kuna watu ambao wanafanya hila ili kuwakwamusha katika zoezi la uchangiaji wa fedha ili kuwatoa viongozi nane wa Chadema Gerezani.
“Kuna watu wente Mkereketo wa nafsi, muwasho wa moyo, chuki binafsi, kinyongolilo na roho nyeusi ya zopata wanafanya hila na propaganda ili kutukwamisha,” aliandika Profesa Jay.
Profesa Jay aliandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa
” Niwahakikishie tu kuwa Mungu sio kiziwi wala sio kipofu hamtafanikiwa, tuendelee kuchanga kwa wingi hii ndio nguvu ya umma,”
Kuna watu wenye Mkereketo wa Nafsi, Muwasho wa Moyo, Chuki binafsi, Kinyongolilo na Roho Nyeusi ya ZOPATA wanafanya HILA na propaganda ili kutukwamisha, Niwahakikishie tu kuwa Mungu sio KIZIWI wala sio KIPOFU, HAMTAFANIKIWA, Tuendelee Kuchanga kwa wingi, Hii ndio NGUVU ya UMMA💪🏻 pic.twitter.com/01xHAtbCrE— Joseph L. Haule (@ProfessorJayTz) March 11, 2020
No comments