Header Ads

Header ADS

Rais Magufuli amtaka Waziri Mwakyembe kubeba aibu ya Serengeti Boys

Rais John Magufuli amesema huwa anajisikia vibaya na kuhuzunishwa na kushindwa kufanya vizuri kwa Timu ya Taifa ya Vijana Tanzania. 


Katika ziara yake mkoani Mbeya ameeleza kutofurahishwa kwake na matokeo ya AFCON U17 ambapo Tanzania (Serengeti Boys) ilishindwa kufuzu michuano hiyo. 


Amemtaka Waziri wa Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kuibeba aibu hiyo na kumtaka alitafakari suala hilo. 


"Lakini katika vitu vinavyoni 'bore' ni kufungwa huwa najisikia vibaya. Haiwezekani, uwanja wa kwako, nchi ina idadi ya watu milioni 55 tukiwa tunafungwa ni sisi wote tumefungwa, labda kufungwa nako ndiyo mchezo wenyewe," amesema. 


Utakumbuka leo katika ziara yake mkoani Mbeya Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba za walimu, mabwenu na maabara katika Chuo cha Ualimu Mpuguso na kuzungumza na wananchi wa Tukuyu.



No comments

Powered by Blogger.