Amwagiwa Mafuta ya Taa na Kuchomwa Moto ili Kuondoa Mapepo
Phillipo Elias (22), mkazi wa kijiji cha Musati Wilayani Serengeti, ameunguzwa moto mwilini wakati akiombewa kanisani ili aponywe maumivu ya kichwa kwa kumwagiwa mafuta ya taa na kupigwa kiberiti kama njia ya kumfanyia ibada ya kumtoa pepo
Kwa mujibu wa maelezo yake, tukio hilo lililotokea juzi, lilifanywa na mchungaji wa Kanisa la Cag Calvary, Anna Butake ambaye amekana kumchoma moto muumini huyo akisema hajui kilichotokea hadi Phillipo akaungua kwasababu yeye alilenga kuchoma moto nguo zilizoonekana kuwa na zindiko
Philipo anasema alikwenda kwa mchungaji huyo kwa ajili ya maombi kutokana na kumfahamu akidai wanatoka wote Kigoma na kupata taarifa kuwa ana nguvu za uponyaji
Mkuu wa Polisi Wilayani Serengeti, Mathew Mgema alisema wanafuatilia na kuchunguza kwa makini tukio hilo ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria
No comments