Pasta Azindua Chupi zenye Sura yake Kuwasaidia Warembo "Singo' Kupata Waume
Pasta mmoja nchini Nigeria amezindua chupi na sindiria zenye chapa ya picha yake ili kuwasaidia wanawake waseja wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.
Pasta Dr J.S. Yusuf alisema aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za 'baraka' ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.
Kulingana na pasta Dr J.S. Yusuf, ambaye ni mkuu wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International mjini Abuja, aliagizwa na Mungu kuzindua chupi hizo za 'baraka' ili kufungua milango ya ndoa Mwaka Mpya.
Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema “Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.”
Chupi hizo zinasemekana pia kuwasaidia wanawake kupigana na magonjwa na kupata bahati njema wakiwa na wanaume na kuwafanya kuwaposa.
Magazeti Ijumaa, Disemba 31: Magoha Aagiza Wanafunzi Mashoga Wafukuzwe Katika Shule za Bweni
Pasta adai kuwa na mpango wa kando si dhambi
Itakumbukwa kwamba si mara ya kwanza kwa watumishi wa Mungu kufanya mambo ya kiajabu.
Mhubiri ambaye ni raia wa Ghana, Osofo Acheampong, alitoa kauli nzito kwa kusema kwamba sio vibaya kwa mwanamume kuwa na mpango wa kando hata ingawa ni mume wa mtu.
Pasta Acheampong, anayesemekana kuwa kiongozi wa Kanisa la Kipentekosti la Sabato, alitoa maoni hayo kwenye mahojiano ya hivi punde huku akitoa mafungu ya Bibilia kuipa uzito kauli yake.
Nabii Owuor ajitokeza na Miujiza yake Nakuru
Kwingineko humu nchini, baada ya kuingia chini ya maji tangu mlipuko wa COVID-19, Nabii wa Mungu David Owuor amejitokeza tena hadharani mara ya kwanza.
Mwanzilishi huyo wa Kanisa la Repentance and Holiness Ministry, anatarajiwa kuandaa mkutano mkubwa wa maombi katika uwanja wa Menengai jijini Nakuru.
Askofu Isaak Suter, ambaye ni mshauri wa ndoa katika kanisa hilo, alisema kuwa magonjwa yataponywa wakati wa ibada hiyo, na viwete pia watatembea.
No comments