Header Ads

Header ADS

Mwigizaji The Rock Ajitoa Kuigiza Filamu ya Fast & Furious Sehemu ya 10


Muigizaji Dwayne Johnson maarufu kama the “The Rock” amekataa ombi la kurejea kuigiza muendelezo wa filamu ya Fast & Furious sehemu ya 10.

The Rock katika interview yake na CNN iliyochapishwa siku ya jana amekataa ombi la Vin Diesel kurejea katika Fast & Farious na kumkosoa kwa kitendo chake cha kuongolea suala hilo katika mitandao ya kijamii kwa kuwahusisha watoto na marehemu Paul Walker.

“Nilishangazwa sana na post ile ya Vin Diesel, mwezi wa sita mwaka huu niliongea nae faragha na kumwambia sitaweza kuigiza tena filamu hiyo ila nitatoa ushirikiano wangu katika kuandaa filamu hiyo ili kuhakikisha inafanikiwa na hata washirki wengine wote niliongea nao na walinielewa,” Majibu ya The Rock.



No comments

Powered by Blogger.