Maiti 200 zafukuliwa Dar es Salaam
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imeanza kufukua makaburi zaidi ya 200 yaliyopo katika Mtaa wa Butiama, Kata ya Vingunguti ili kuyanusuru kutokana na kubomoka kwa kingo za Mto Msimbazi.
Kazi ya ufukuaji miili hiyo imeanza leo, ambapo mamia ya wananchi walijokeza kufukua ndugu zao na hivyo kusababisha simanzi kutawala katika eneo hilo.
Akizungumza katika eneo la tukio, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto,alisema miili hiyo itazikwa upya katika eneo la Mwanagati.
“Tufukua miiili 200 kutoka makaburi haya ya Butiama, yaliyopo katika Kata ya Vingunguti kwenda kuzikwa upya katika eneo la Mwanagati.
Kulikuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kutokana na Mto Msimbazi kubomoa makaburi haya na miili kuondoka na maji,” alisema Kumbilamoto.
Alisema awali Jiji la Dar es Salaam, lililenga kufukua makaburi 189 lakini kutokana na wananchi wengi kujitokeza kuomba ndugu zao walio zikwa katika eneo hilo kufukuliwa na kuhamishwa hivyo huenda idadi ya miili kufukuliwa ikafikia 220.
No comments