Habari za Zuchu na Diamond Platnumz Zashtua Wengi
MIONGONI mwa habari zinazoshtua zaidi kwa sasa ni madai ya staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz kudaiwa kuwa mbioni kumuoa msanii wake, Zuchu @officialzuchu.
Kwa mujibu wa ubuyu huo, kwa muda mrefu wawili hao wamekuwa na ukaribu wenye shaka na viulizo vingi Hata hivyo, baadhi ya wanamitandao hawaamini kwa sababu wanaamini Diamond @diamondplatnumz ana mchumba wake mwingine aliyeko Afrika Kusini kulingana na watu wake wa karibu akiwemo Juma Lokole.
Wengine ambao walionekana kusoma habari walishindwa kuacha kushangaa jinsi watu hao wanaodaiwa kuwa wapenzi waliweza kuficha uhusiano wao kutoka kwa umma kwa muda mrefu.
Wasanii hao wawili hawajajitokeza kuthibitisha habari hizo, lakini mashabiki na wanamitandao wamesalia na maswali chungu nzima, je, ukweli ni upi?
No comments