Drake Agawa Pesa Barabarani
Rapa maarufu Duniani kutoka nchini Marekani, Aubrey Drake Graham ‘Drake’ ambaye ni mzaliwa wa Canada ameitumia siku ya boxing day kugawa pesa pesa kwa watu mbalimbali barabarani huko kwao, Toronto nchini Canada.
Drake ameposti video mbili kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii zikimuonesha akifanya zoezi hilo.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja ni kiasi gani cha pesa alichogawa; lengo likiwa ni kuonesha ukaribu alionao na watu wake wa Toronto.
No comments