Simba na Yanga kukutana tena septemba 25
WATANI wa jadi Simba na Yanga wanatarajiwa kukutana kwa mara nyingine tena Septemba 25, Uwanja wa Mkapa.
Mchezo huo utakuwa ni wa Ngao ya Jamii ambapo unatarajiwa kuchezwa saa 11:00 jioni Uwanja wa Mkapa.
Itakuwa ni mara ya tano kwa watani hao kukutana ndani ya uwanja kwa mwaka 2021 jambo ambalo ni rekodi kwa miamba hii miwili.
Ni mara mbili walikutana katika Ligi Kuu Bara ambapo Mchezo wa kwanza waligawana pointi mojamoja na ule wa pili Yanga ilisepa na pointi tatu mazima kwa ushindi wa bao moja kwa nunge.
Pia walikutana katika Kombe la Mapinduzi, Zanzibar na Yanga ilisepa na taji kwa ushindi wa penalti kwa kuwa ilikuwa ni fainali.
Mara ya nne ilikuwa fainali ya Kombe la Shirikisho na Simba ilishinda kwa bao 1-0, Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma
No comments