Naibu Mkuu wa Polisi Uganda, Paul Lokech afariki
JESHI la Polisi nchini Uganda UPDF limethibitisha kifo cha Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Meja Jenerali Paul Lokech. Msemaji wa Jeshi la UPDF Brig. Flavia Byekwaso ameandika katika mtando wake wa kijamii wa Twitter kuwa Jenerali Lokech amefariki leo siku ya Jumamosi.
Kifo chake kimetokana na shinikizo la moyo (Blood Clot) lakini taarifa zaidi kuhusu kifo chake itatolewa hapo baadaye na jeshi la polisi. Jenerali aliteuliwa kuwa naibu wa mkuu wa jeshi la polisi mwezi wa Desemba mwaka 2020 kuchukua nafasi ya Meja Stephen Muzeeyi Sabiiti baada ya kuondolewa na Rais Museveni.
Lokech anakumbukwa zaidi alipokuwa Mogadishu nchini Somali chini ya kikosi cha UPDF aliweza kuyatawanya makundi ya Alshabaab mji kuu wa Mogadishu Somali. Kifo chake kimetokea wiki moja baada ya kifo cha Jenerali Pecos Kutesa ayelifariki nchini India akipewa matibabu. Lokech alikuwa miongoni mwa majenerali wadogo zaidi jeshini.
No comments