Nabii Bendera Awachana Wanasiasa na Wachungaji
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Ufunuo, Bishop Paul Bendera amewashukia baadhi ya viongozi wa siasa wenye tabia za kuongea ongea na viongozi wa dini wanaongea ongea akidai kuwa ni waongo na wanataka kupata mtaji wa watu kwa njia za udanganyifu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Askofu Bendera amesema;
Nina mambo mbili muhimu ya kushauri:
1. Kwa wanasiasa
Usimfanyie hila kiongozi aliyeko madarakani kwa kumzunguka. Atakaye umia ni wewe usiyepo madarakani
2. Kwa watumishi wa Mungu
Ukifanya mbinu ya kukuza kanisa kwa kushirikiana na wanasiasa, mbinu hiyo haitofichika.
Mwanadamu ana asili ya kufanya research ya kauli za watu na malengo ya kauli hizo. Na jibu atakalolipata atapata malengo yako na mipango yako hata asipomuuliza mtu. Ni mara chache sana mtu mtulivu afanye research na akafeli.
Nimeshawafanyia research wanasiasa wengi wanaoongea ongea sana. Malengo yao huwa ni kugombea nafasi za juu ama kuteuliwa. Na asili yao ni waongo. Watumishi wengi wa Mungu wanaongea ongea huwa hawaogopi kudhalilika bali huangalia namna ya kupata watu kwa njia ya udanganyifu.
No comments