Kimeumana Ufanransa, Ngumi Zapigwa Uwanjani
GAME ya Ligi kuu ya Ufaransa (Ligue 1) kati ya Timu ya Nice dhidi ya Marseille umeshindwa kumalizika baada ya mashabiki wa Nice kufanya vurugu na kuingia uwanjani.
Mashabiki wa Nice waliingia uwanjani baada ya Dimitri Payet wa Marseille kukasirika na kuwarushia chupa ya maji mashabiki hao waliokuwa wamempiga na chupa hiyo.
Mchezo huo ulisimama dakika ya 74 ambapo Nice ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0, baadhi ya wachezaji wa Marseille Luan Peres na Matteo Guendouzi wameumia shingoni wakati wa purukushani hizo.
No comments