Kauli Ya kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge Baada ya Kumaliza Kumhoji Askofu Gwajima
Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amehojiwa kwa zaidi ya saa mbili na kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge huku shauri lake likitarajiwa kuendelea kesho kutwa.
Akizungumza mara baada ya mahojiano hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Emmanuel Mwakasaka amesema wamemaliza kusikiliza shauri la Askofu Gwajima kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili itafanyika kesho kutwa.
“Askofu Gwajima ametoa ushirikiano wa kutosha bado suala hili linaendelea kazi yetu kama kamati ni kuchunguza Mbunge anayekiuka maadili na kanuni za bunge tumemruhusu aende lakini shauri lake bado linaendelea,”- Amesema
Mwenyekiti huyo amesema kwa sasa hawawezi kusema kama akikutwa na hatia atachukulia hatua gani au kupewa adhabu gani kwakuwa zipo nyingi na mwenye kazi hiyo ni Spika wa Bunge pekee yake.
No comments