Beki wa klabu ya Simba Joash Onyango na Victor Wanyama watemwa Kenya
Shirikisho la soka la Nchini Kenya kikosi cha awali chenye orodha ya wachezaji 36 huku majina makubwa, Jina la nahodha Victor Wanyama na beki kitasa wa klabu ya Simba, Joash Archieng Onyango yakitemwa kikosini.
Harambee Stars ipo kundi E na timu za Mali, Uganda na Rwanda zikiwania nafasi ya kuliwakilisha bara la Afrika kwenye michuano ya kombe la Dunia 2022 nchini QATAR.
Kenya itacheza dhidi ya Uganda Septemba 3, 2021 katika uwanja wa Nyayo nchini Kenya na Septemba 7, 2021 itakipiga ugenini dhidi ya Rwanda.
Baada ya kikosi hicho kutajwa, Kocha wa timu ya taifa ya Kenya, Jacob Mulee 'GHOST' amesema, " Hiki ni kikosi cha wachezaji imara, tuna eneo kubwa la uzoefu, vijana na uwezo mkubwa. Hili ni kundi la wachezaji ambao wanastahili na kuwa na kitu cha kujivunia kuanza mbele ya Uganda na kuendelea".
Magolikipa.
Ian Otieno (Zesco United, Zambia), James Saruni (Ulinzi Stars, Kenya), Joseph Okoth (KCB, Kenya), Brian Bwire (Kariobangi Sharks, Kenya), Brandon Obiero (Kariobangi Sharks)
Walinzi.
Joseph Okumu (KAA Gent, Belgium), Eric Ouma (AIK, Sweden), Eugene Asike (Tusker, Kenya), Nashon Alembi (KCB, Kenya), Harun Shakava (Gor Mahia, Kenya), Andrew Juma (Gor Mahia, Kenya), Siraj Mohammed (Bandari, Kenya), Clyde Senaji (AFC Leopards, ), Frank Odhiambo (Gor Mahia, Kenya), Bolton Omwenga (Nairobi City Stars, Kenya), Daniel Sakari (Kariobangi Sharks, Kenya), Baraka Badi (KCB, Kenya)
Viungo.
Richard Odada (Red Star Belgrade, Serbia), Duke Abuya (Nkana, Zambia), Duncan Otieno (Lusaka Warriors, Zambia), Lawrence Juma (Sofapaka, Kenya), Kenneth Muguna (Azam, Tanzania), Kevin Kimani (Wazito, Kenya), Patillah Omoto (Kariobangi Sharks, Kenya), Enock Momanyi (FC Talanta, Kenya), Jackson Macharia (Tusker, Kenya), Eric Johanna (Jonkopings Sondra IF, Sweden), Boniface Muchiri (Tusker, Kenya), Abdalla Hassan (Bandari, Kenya)
Washambuliaji.
Michael Olunga (Al-Duhail, Qatar), Masud Juma (Difaâ Hassani El Jadidi, Morocco), Cliffton Miheso (Gor Mahia, Kenya), Erick Kapaito (Kariobangi Sharks, Kenya), Elvis Rupia (AFC Leopards), Samuel Onyango (Gor Mahia, Kenya), Benson Omalla (Gor Mahia, Kenya)
Wataanza rasmi Agosti 24, 2021 kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani na Agosti 30 kwa wachezaji wanaocheza ligi za nje.
No comments