ACT yatoa neno kodi ya miamala na majengo
Chama cha ACT-Wazalendo kimetoa mapendekezo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mapitio ya kodi ya majengo kupitia luku na tozo ya miamala ya simu ili kuwaondolea mzigo mzito wa kodi wananchi masikini.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika ofisi za chama,Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu amesema serikali inapaswa kuwasaidia wananchi kutoka kwenye hali ngumu iliyosababishwa na athari ya janga la Corona.
Akitoa mapendekezo yao Ado amesema kabla ya zoezi la ukusanyaji fedha kuanza rasmi serikali ilipaswa kufanya utambuzi wa luku zinazopaswa kukatwa kodi hiyo ili kuepusha kukata watu kodi kimakosa huku akigusia suala la mwenye nyumba na mpangaji kuwa mpangaji hawezi kumwajibisha mwenye nyumba.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA ikijibu juu ya nani ana wajibu wa kulipa kodi ya jengo imesema kodi hii inalipwa na mmiliki wa jengo na si mpangaji na endapo mpangaji atalipia wakati wa kununua umeme awasiliane na mwenye nyumba ili arejeshewe fedha yake na kuainisha mita moja itakayo katwa kodi hiyo kila mwezi.
No comments